Mwenyekiti wa Asasi (Tanzania Mjini Kazi) akitoa historia fupi ya Asasi hiyo kwa waandishi wa habari (kulia) pamoja na kutambulisha wajumbe wa Asasi na Wakuu wa Idara zinazopatikana katika Asasi hiyo.
Katika kutambulisha Asasi hiyo Mwenyekiti huyo (Daud Salum) alisema kuwa ,Asasi ina idara kuu tano ambapo alizibainisha na kueleza kazi za kila idara.
Hatua hiyo ilienda sambamba na kuwatangaza wataalamu au wakuu wa idara ambao anasema wataalamu hao wamejiandaa katioka nyanja zote na wako tayari kufanya kazi na Asasi ili kufanikisha malengo ya Asasi.
Idara hizo:- Idara ya Rushwa na Madawa ya kulevya, Idara ya Kilimo na Mifugo, Idara ya Mazingira, Idara ya Ujasiliamali, Idara ya Uwezeshaji pamoja na Idara inayohusika na kutoa elimu juu ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Pia Katibu Mkuu wa Asasi hiyo Ndugu Paulo Masenga(kushoto) alipata fursa ya kusisitiza mambo ya msingi na mikakati ya Asasi hiyo katika kuleta maendeleo kwa jamii na kufanya Morogoro kuwa Jiji
Waandishi wa habari walipokuwa wanasikiliza Hotuba za viongozi wa Asasi katika viwanja vya Midland Hotel